Mahakama ya Rufani nchini Kenya imefuta nyongeza ya mishahara ya walimu ya hadi asilimia 60 iliyokuwa imeamliwa na mahakama ya Mizozo ya Wafanyakazi.

Majaji waliosikiliza kesi hiyo wameeleza kuwa uamuzi uliofanywa na mahakama ya Mizozo ya wafanyakazi ilikiuka katiba ya nchi hiyo na kwamba kabla ya kutoa uamuzi huo ilipaswa kufanya mashauriano na kamati ya Mishahara na Marupurupu.

Walimu Kenya

Walimu nchini humo waliendesha mgomo uliodumukwa muda wa wiki tano mfululizo uliopelekea shule zote za umma kufungwa. Hata hivyo, serikali ya Rais Uhuru Kenyatta ilikataa kuwaongeza mishahara walimu hao licha ya kuendesha mgomo.

Walimu hao walirejea mashuleni baada ya mahakama ya Mizozo na Kazi kuwataka kufanya hivyo na umuzi wake kuwapa faraja ambayo hata hivyo imezimwa na Mahakama ya Rufani.

Hata hivyo, wawakilishi wa walimu nchini humo wameeleza kuwa hawakuridhishwa na uamuzi wa mahakama hiyo na wamepanga kukata rufaa kwenye mahakama za juu zaidi. Hii ina maanisha kwamba kesi hiyo huenda ikapelekwa kwenye Mahakama ya Afrika.

Masanja Mkandamizaji Aanza Rasmi Safari ya Kuingia Bungeni
Urusi yapinga Ripoti ya Marekani kuanguka ndege ya Nchi hiyo, Putin Afanya Maamuzi Magumu