Baada ya tukio la shule ya Sekondari Lindi kuungua moto ambapo jumla ja madarasa 9 na viti na meza zaidi ya 300, Ofisi 4 na vyoo matundu 24  viliteketea na moto uliotokana na hitilafu ya Umeme, Shirika la hifadhi ya taifa ya jamii (NSSF) ikishirikiana na ofisi ya mkoa wa Lindi imechanga jumla ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya kuchangia harambee ya kusaidia ujenzi wa shule ya sekondari ya Lindi iliyoungua moto wiki iliyopita.

NSSF LINDI  (9)

Kufuatia Harambee iliyoongozwa na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa, mkurugenzi mkuu wa NSSF akiwakilishwa na meneja wa mkoa, Bi Nour Aziz ametoa ahadi hiyo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

NSSF LINDI  (4)Wadau mbali mbali walihudhuria harambee hiyo akiwemo mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne, Mama Salma Kikwete ambapo jumla ya Shilingi milioni 80 taslimu zilichangwa huku ahadi na vifaa vya ujenzi zikifikia Shilingi milioni 640 ambapo katika ujenzi mpya Waziri Mkuu ameagiza kujengwa jengo la ghorofa litakalokuwa na ofisi na madarasa.

NSSF LINDI  (8)Baadhi ya Vifaa Ikiwemo Saruji Vilivyotolewa na Wadau Mbalimbali Kuchangia Ujenzi mpya wa Shule ya Sekondari Lindi

 

Ratiba Ya VPL 2016-17 Yavuja, Young Africans Kuanza Na Kiporo
BAVICHA wavimba tena, ‘hatuogopi’