Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa mikoa kuzisimamia halmashauri nchini ili kuhakikisha zinaandaa maeneo mazuri yanayofikika na wateja kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo.

Majaliwa ameyasema hayo leo Jumatatu Oktoba 4, 2021 wakati akifungua kongamano la tano la uwezeshaji lilloandaliwa na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (Neec).

“Tumeagiza halmashauri yetu kuandaa maeneo mazuri ya kufanya ya biashara kwa wafanyabiashara wadogo wadogo. Sio kila eneo linalofaa kwa biashara. Ni maeneo mazuri, yanayofanya biashara na wateja wakafika kupata huduma hiyo,”amesema Majaliwa.

Aidha Amewaagiza wakuu wa mikoa kuzisimamia halmashauri ili kuhakikisha kuwa zinapata maeneo mazuri ya kufanyia biashara.

Majaliwa amesema kuandaa maeneo hayo apo wataratibu taasisi za fedha ili ziweze kuwafikia wafanyabiashara katika maeneo hayo na kuwapa mitaji kwa urahisi.

Amewaagiza wakuu wa mikoa kuzisimamia halmashauri ili kuhakikisha kuwa zinapata maeneo mazuri ya kufanyia biashara.

Majaliwa amesema kuandaa maeneo hayo apo wataratibu taasisi za fedha ili ziweze kuwafikia wafanyabiashara katika maeneo hayo na kuwapa mitaji kwa urahisi.

Facebook, WhatsApp, Instagram zatoweka 'duniani', nini chanzo?
Bilioni 6.3 kukarabati vivuko