Waziri wa Nishati, January Makamba amewataka Wakandarasi wazawa waliopewa kazi katika mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda kujelekea Chongoleani Mkoani Tanga kufanya kazi kwa weledi ili kuleta uaminifu.

Makamba ameyasema hayo katika ziara yake maalumu ya kutembelea eneo kinapojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza mabomba yatakayotumika kusafirisha mafuta ghafi ya mradi huo.

Amesema, “Kiwanda hiki kinachojengwa katika Kijiji cha Sojo Kata ya Igusule, wWlayani Nzega Mkoani hapa, kinatakiwa kukamilika haraka kwa ubora na weledi unaotakiwa ili kazi ianze kutokana na umuhimu wake kwa uchumi wa taifa.”

Aidha, Waziri Makamba ameongeza kuwa makampuni ya ndani yanayoshiriki katika miradi mikubwa kama hiyo wanapata uzoefu na nchi kunufaika ingawa suala la kuchelewesha kazi hukwamisha juhudi za serikali na kuondoa uaminifu.

 ‘Miradi huu una manufaa makubwa kwa serikali, hivyo wakandarasi wa ndani wanaposhirikishwa wanapaswa kufanya kazi kwa weledi na viwango ili iwe rahisi kupata kazi nyingine zinazotekelezwa hapa nchini’,” amebainisha Waziri Makamba.

Hata hivyo, amesema matarajio ya serikali ni kuona mradi huo kuanza kazi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, ambapo pia ameagiza kila mkandarasi aliyepewa kazi katika mradi huo kutimiza wajibu wake ipasavyo.

Ujenzi huo wa bomba hilo la mafuta lina urefu wa kilometa 1,443 zikiwemo 1,115 zitakazojengwa ndani ya ardhi ya Tanzania ambapo mradi huo utagharimu Dola za Marekani bilioni 3.55/- na unatarajiwa kusafirisha mapipa laki 2 ya mafuta kwa siku na wakati wa ujenzi ajira kati ya 6,000 mpaka 10,000 zilitarajia kuzalishwa.

Prof. Ndalichako asimama na madereva
Serikali, TUCTA kujadili nyongeza ya mishahara