Hatiamaye Makampuni matano yanayomilikiwa na mfanyabiashara Yusuf Mehbub Manji yameondolewa katika jengo la Quality Plaza linalomilikiwa na Shirika la Hifadhi ys jamii PSPF.

Jengo hilo lipo kitalu Na.189/2 na liko makabala na Barabara ya Nyerere jijini Dar-es-salaam.

Sababu inayotajwa ya makampuni hayo kuondolewa katika jengo hilo ni deni la kodi ya pango linalofikia kiasi cha shilingi bilioni 13.

Hatua ya kung’olewa makampuni hayo katika jengo hilo ambalo ni mali ya mfuko wa pensheni wa watumishi wa Umma ni baada ya mpangishaji kushindwa kuondoka kwa hiari baada ya kupewa saa 24.

#HapoKale
Majaliwa amaliza mgogoro wa ardhi Manyara Ranch, Akabithi hati kwa Mkurugenzi