Jeshi la polisi Mkoa wa Ilala  linamshikilia kijana mmoja  kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa udanganyifu kwa kutumia jina la Mkuu wa Mkoa  wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda juni 16 mitaa ya Samora.

Akitoa taarifa kwa wanahabari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala ACP Salum R Hamduni amesema kuwa  mtuhumiwa alikamatwa baada ya kupiga simu kwa Mkurugenzi wa JONES LOGISTICS LTD Bw. James Lupondo akihitaji mchango wa dola 3500 za kumsaidia mwanafunzi aliyepata ufadhili wa kusoma nchini Ufilipino.

_DSC2012

Akiendelea kufafanua Kamanda Hamduni amesema kuwa mtuhumiwa huyo alidai kijana anayehitaji msaada angefika ofisini kwake baaada ya masaa  mawili akiwa na nyaraka zote hivyo makabidhiano ya fedha angehitaji yafanyike kupitia bank ya ECO BANK Dar es salaam, akaunti ya Kenya  huku akitoa namba ya simu ya kijana huyo ni 0717338473.

Hata hivyo Jeshi la polisi linatoa rai kwa wananchi wote kuwa makini na kwamba utapeli kwa kutumia majina ya viongozi umeshika kasi na kusema muathirika mwingine katika matukio hayo ya kuchafuliwa majina  ni pamoja na Waziri Mkuu  wa Tanzania Mh. Majaliwa K Majaliwa

Sanjari na hayo mtuhumiwa bado yupo  anahojiwa ili kuweza kuwatambua wengine anaoshirikiana nao katika utapeli wa namna hiyo na pindi upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani, huku raia wema wakiombwa kuendelea kutoa taarifa za kukamata wahalifu.

 

Zaidi ya Watu 30 Wauawa Libya
Young Dee akiri kutumia dawa za kulevya, aomba radhi