Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara jana alitumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe ulioleta tafsiri tofauti kwa baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wakidhani kuwa Manara anampango wa kuondoka klabu hiyo.

Tafsiri hiyo ni kufuatia ujumbe uliosomeka;

“Nia yangu ni njema sana lakini na mimi nina nyongo sihitaji heshima ila walau nipewe utu ninaostahili nimefanya kwa kadiri nilivyojaaliwa na Mungu ila lazima tusonge mbele kwa maslahi mapana ya klabu.”

Mapema leo hii amewatoa hofu mashabiki wake na kusema kuwa hawezi kuhama klabu hiyo kwani ni dhahiri kuwa yupo sehemu sahihi na anafanya kazi mahali sahihi kwa wakati sahihi, na hivyo kwa sasa Simba ipo katika wakati muhimu.

kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram, Manara ameandika.

“Siondoki Simba na naomba muelewe hvyo ninafanya kazi sehemu sahihi na wakati sahihi….rafiki zangu na washabiki wa klabu muelewe hvyo..walichokitangaza ni uzushi…nawezaje kuwaacha simba kipindi hiki muhimu”?

Aidha Simba kwa sasa wamebakiza point tano kuwa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Soka Tanzania, mara baada ya kuishinda timu ya watani wao wa jadi, Yanga mara baada ya kuwafunga goli moja la kichwa katika mchuano mkali uliopigwa uwanja wa taifa, Dar es salaam siku ya jumapili iliyopita ya tarehe 29 Aprili 2018.

 

Msigwa anena makubwa kuhusu ongezeko la mishahara
Kamati ya wakimbizi Rwanda yavunjwa

Comments

comments