Maafisa usalama wa Marekani Jumapili walilazimika kutumia mabomu ya machozi baridi kuwatawanya wahamiaji waliokuwa wakikaribia kuingia Marekani kutoka Mexico.

Maafisa hao wa kulinda mipaka walifunga barabara ambayo ndiyo kivukio kikubwa zaidi cha wahamiaji wanaoingia Marekani katika juhudi za kukabiliana nao.

Hii ni baada ya Rais Donald Trump kutangaza kwamba utawala wake hauruhusu kuingia Marekani kwa urahisi kama wanavyotaka wahamiaji hao.

Aidha, hali ya wasiwasi imekuwa ikitanda katika eneo hilo, katika siku za karibuni, kufuatia maelfu ya wahamiaji kutoka nchi za Amerika ya Kusini kuwasili kwenye uwanja mmoja wa michezo mjini na Marekani.

Hata hivyo, shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa serikali ya Mexico, ilitangaza kuwa ilikuwa imeuchukua tena udhibiti wa mpaka baada ya takriban wahamiaji 500 kujaribu kuvuka mpaka wa kuingia Marekani kwa nguvu

Florentino Perez ajilipua mkutano wa bodi
Mikoa ambayo magereza yake yatalima Mahindi, Maharage na Mpunga yatajwa

Comments

comments