Mlinda lango la Aston Villa ya England Damián Emiliano Martínez Romero, leo Alfajiri alikuwa shujaa kwa kuibeba timu ya taifa lake la Argentina.

Martínez ambaye alijiunga na Aston Villa akitokea kaskazini mwa jijini London yalipo makao makuu ya Klabu ya Arsenal FC, aliokoa penati 3 katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Colombia.

Ushujaa wa Milinda lango huyo mwenye umri wa miaka 28, umeisaidia Argentina kutinga hatua ya fainali ya Copa America.

Timu ya taifa ya Argentina imefanikiwa kutinga fainali ya Copa América kwa kuifunga timu ya taifa ya Colombia kwa changamoto ya mikwaju ya penati 3-2, baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya kufungana 1-1.

Argentina itacheza fainali dhidi ya wenyeji Brazil walioiondosha Peru kwa kuifunga bao 1-0 usiku wa kuamkia jana Jumanne (Julai 06).

Mchezo wa fainali umepangwa kuchezwa usiku wa kuamkia Jumatatu (Julai 12) saa 10:00 Alfajiri.

Neymar: Mungu amejibu maombi yangu
Limewakuta: Ni polisi wazungu waliomvua nguo zote mwanamke mweusi mlemavu