Kundi la Wataalamu huru wa Haki za Binaadamu la ‘The Interdisciplinary’ – GIEI, nchini Mexico limeikosoa Serikali ya nchi hiyo kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya waliohusika na mauaji ya wanafunzi 43 mwaka 2014, licha ya uchunguzi kuwataja wahusika.

Wataalamu hao wa GIEI, wamesema mamlaka za nchini Mexico zimeshindwa kutekeleza agizo la waendesha mashtaka la kukamatwa kwa waliohusika na kupotea kwa wanafunzi hao, huku jeshi likibana ufikiaji wa taarifa na Habari muhimu.

Wamesema, wasiwasi wao ni kuhusu kuendelea kucheleweshwa kwa uchunguzi kuhusiana na kesi hiyo, na kulihimiza Jeshi kuweka utaratibu rafiki wa kutoa taarifa na kufanyia kazi agizo la waendesha mashtaka waliotoa agizo la kukamatwa kwa waliohusika.

Hata hivyo Mjumbe wa GIEI, Carlos Beristain amesema kesi hiyo haiwezi kutatuliwa kwa kuzuia habari au kutoa majibu yasiyolingana na ukweli, huku mjumbe mwingine wa GIEI, Angela Buitrago akisema baadhi ya maafisa wa umma ambao maagizo ya kukamtwa kwao yalitolewa miezi sita iliyopita, bado hawajakamatwa.

Utani wa Papa akitoka Hospitali: Asema bado yupo yupo sana
Wagonjwa zaidi ya 400 wapatiwa matibabu ya kibingwa