Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kuwa chama chake kiko tayari kusitisha mikutano na maandamano ya Septemba 1 yaliyotajwa kuwa sehemu ya Operesheni UKUTA, endapo yataanzishwa mazungumzo kutafuta muafaka.

Freeman Mbowe akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chadema, Kanda ya Kaskazini

Freeman Mbowe akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chadema, Kanda ya Kaskazini

Mbowe ambaye hivi sasa yuko kanda ya Kaskazini akipanga mikakati na viongozi wa chama hicho kuhusu namna ya kuratibu na kutekeleza operesheni UKUTA, amesema kuwa wako tayari kusitisha mpango huo na kushiriki mazungumzo yoyote yatakayoanzishwa.

“Tutashiriki mazungumzo yoyote ya kusaka muafaka na kama matamko ya Rais Magufuli yakibalishwa. Tutawaeleza wanachama kusitisha mikutano ya Septemba 1 na kuendelea na mikutano ya kawaida,” alisema Mbowe.

Baadhi ya viongozi wa Chadema Kanda ya Kaskazini wakimsikiliza Mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe

Baadhi ya viongozi wa Chadema Kanda ya Kaskazini wakimsikiliza Mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe

Kiongozi huyo wa Chadema alitangaza kufanyika kwa Operesheni Ukuta nchi nzima na kwamba Kamati Kuu ya Chama hicho imeridhia kufanya maandamano na mikutano nchi  nzima kwa lengo la kupinga kile walichodai ni kuminywa kwa demokrasia ndani na nje ya Bunge.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amewataka kusitisha maandamano hayo akieleza kuwa kama walizoea kutikisa kiberiti, wakati huu hiki ni kiberiti cha gesi.

Waliopewa uraia na kuutumia vibaya kunyang’anywa na kurudishwa walikotoka
Picha: Ziara ya Waziri Mkuu Mpanda