Mbunge wa zamani wa Jimbo la Ngorongoro Mkoani Arusha Kaika Ole Telele ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika Serikali ya awamu ya nne ameeleza kuwa ameamua kufanya maamuzi ya kuhamia Msomera ili kupunguza shughuli za kibinadamu ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Kwa mujibu wa Gazeti la Habari leo, Telele amesema yuko tayari kuhamia Kijiji cha Msomera Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga kwa hiari kuungana na wananchi wengine ambao wameshahamia.

“Nimeona ni kweli idadi ya watu na mifugo ndani ya Hifadhi imeongezeka, nimehamasika baada ya kuona zoezi hili ni la hiari na Serikali yetu imeboresha miundombinu muhimu kule Msomera Handeni,”

“mimi binafsi nimetafakari na kwa hiari yangu mwenyewe nimeamua kuondoka ili wengine nao waendeleee kuhamasika na kuunga mkono zoezi hili muhimu ambalo linaendeshwa kwa amani na utulivu kabisa,” amesema Telele.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela ameeleza kuwa zaidi ya kaya 25 kutoka ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro zinatarajia kuhama kwa hiari kwenda Kijiji cha Msomera Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Juni 30, 2022.

Bernard Morrison aomba jezi 100 Simba SC
Wadaiwa sugu mapato ya ndani wawakiwa moto