Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel ameagiza kukamatwa wadaiwa sugu wa makusanyo ya Mapato ya ndani shilingi Milioni 48 na kuhakikisha wanarejesha fedha hizo ndani ya mwezi mmoja Wilayani Misungwi.

Mhandisi Gabriel ametoa agizo hilo wakati wa Mkutano maalum wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo lililofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri kwa ajili ya kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022.

Amewataka Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kuhakikisha Watumishi hao wanaodaiwa fedha hizo wanarejesha mapema fedha za Serikali ambapo waangalie pia mikataba yao na kuona Wadhamini wao ili waweze kutoa fedha za makusanyo ya  mapato ya ndani wanayodaiwa ili ziweze kutumika kuleta maendeleo kwa Wananchi wa Misungwi.

Amesema kwamba  fedha za mapato ya ndani shilingi 48,316,205/=  zilizokusanywa kwa nyakati tofauti na Wakusanya mapato wa Halmashauri hiyo wakiwemo Watumishi na  wakusanyaji wengine wa mapato walioingia mikataba ya kukusanya mapato husika.

“Lazima msome tabia za wakala wanaokusanya fedha za mapato na kujiridhisha na uhalali na  nyendo zao na kuhakikisha wanajiridhisha fedha za mapato kwa wakati,” amesisitiza Mhandisi Gabriel.

Ameeleza kuwa vyombo vya uchunguzi wawasake wote na warejeshe fedha zote za makusanyo ya mapato ya ndani  na kuwataka Watumishi wote wanaodaiwa fedha za mapato wakatwe kutoka katika mishahara yao pia wajiridhirishe katika kudhibiti fedha za mapato yasivuje na kuimarisha mifumo na kuweka  mikataba makini na kuagiza suala hilo lishughulikiwe kwa wakati ndani ya mwezi mmoja.

Kwa upande wake Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi limeridhiria agizo hilo la Mkuu wa Mkoa  la  kuwakamata wadaiwa sugu wa  makusanyo ya fedha za mapato pamoja Wadaiwa wa madeni ya mikopo ya Vikundi vya Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu ambazo ni fedha za Vikundi shilingi milioni 83.9 ambazo walikopeswa kwa muda lakini hawajweza kurejesha fedha hizo kwa wakati.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi wakinyosha mikono ishara ya kuridhia maelekezo na maagizo ya Mhe, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika Mkutano wa Braza la Hoja za Mdhbiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za mwaka 2020/2021 za Halmashauri ya Wilaya hiyo

Awali akiwasilisha taarifa ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2020/2021 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Benson Mihayo  amesema kwamba  katika ukaguzi huo Halmashauri hiyo  imepata Hati ya kuridhisha ambapo hoja zilizohojiwa kwa mwaka wa fedha 2020/2021 zinaendelea kutekelezwa.

Mbunge wa zamani Ole Telele kuhamia Msomera
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Juni 28, 2022 Â