Watu 27 wamefariki dunia baada ya mchungaji wa kanisa la AK Spiritual Christian Church lililopo nchini Zambia, kuwanywesha dawa ya kuondoa madoa ya nguo Jik wakiwa kanisani.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari nchini Zambia zinaeleza mchungaji Phala aliwaambia waumini wake kuwa Jik hiyo inaondoa mapepo hivyo akaanza kuwanywesha kwa nia ya kuwaombea mapepo yao yanayowatesa yawatoke.

Licha ya kuwa tayari waumini 27 wamefariki, waumini wengine 18 hali zao sio nzuri na wamekimbizwa hospitali kupatiwa matibabu.

Aidha afisa wa polisi Limpopo tayari wameanza uchunguzi juu ya tukio hilo, huku wakioneshwa kushangazwa na tukio hilo ambapo miongoni mwa  wliofariki wapo wauguzi wa afya na walimu wa nne.

Wakala wa Serikali mtandao yaja na mfumo mpya
Video: Tanasha ameachia ngoma mpya, Mama Diamond ampa tano, Diamond aufyata

Comments

comments