Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla ametangaza kusitisha likizo za Watumishi wa Umma mkoani humo akiwataka wachape kazi tu!

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu huyo wa Mkoa alieleza kuwa ametoa maelekezo ya kisitishwa kwa likizo za watendaji wote, wakuu wa idara zote na wakurugenzi kwa kuwa anataka wachape kazi tu, kama ilivyo kauli mbiu ya serikali ya awamu ya Tano.

Alipoulizwa kuhusu likizo kuwa haki ya mfanyakazi kisheria, Mkuu huyo wa Mkoa alieleza kuwa kuna Sheria na busara na kwamba yeye atatumia busara zaidi.

“Likizo ni ya kila mtu, mtumishi yeyote.. Agizo langu ni kwa kila mtumishi. Lakini ujue kuna ubinadamu.  Huwezi kusema unaumwa, unauguliwa mtoto au umefiwa (halafu tukunyime likizo).  Lazima ujue kuna Sheria, kanuni, utaratibu na ubinadamu na busara, “alisema.

Makalla alisema kuwa kama Rais John Magufuli alitoka kwenye kampeni tu na kuanza kazi bila kupumzika, sio ajabu kwa watumishi wengine kufanya hivyo.

 

Hapa Kazi Tu: Bandarini Hapapenyeki, Mengine Yanaswa
Navy Kenzo Kuuza Album Yao Mpya Kipekee...