Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, David Silinde amefunga mafunzo ya ufugaji Jongoo Bahari katika Chuo cha Ufundi Stadi – VETA, Kampasi ya Lindi ambayo yaliratibiwa na Wizara hiyo chini ya Wakala ya Mafunzo ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi – FETA, kampasi ya Mkindani – Mtwara.

Akihutubia wakati wa kufunga mafunzo hayo ya siku kumi, yaliyohudhuriwa na washiriki 68 Silinde ametumia fursa hiyo kuwataka watumie ujuzi walioupata kuzalisha Jongoo Bahari, ili kujiongeza kipato chao na kuinua uchumi wa Taifa.

Amesema, “Mafunzo haya ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia aliyoyatoa kwenye kilele cha Maonesho ya Nanenane, mwaka jana Mbeya, ambapo alielekeza sekta zote za uzalishaji ikiwemo Sekta ya Uvuvi kushirikisha Wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi kuwawezesha wananchi waweze kujiajiri.”

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga amewataka wananchi mkoani humo
kuzalisha kwa wingi mazao ya uvuvi, ikiwemo Jongoo Bahari, ili kuendelea kuupandisha uchumi wao na wa Mkoa kwani kilo moja ya Jongoo Bahari hao huuzwa kwa zaidi ya shilingi 180,000.

Uwanja wa Man City kuboreshwa maradufu
Mecky Maxime awashangaa wanaoibeza taifa Stars