Waziri wa Mambo ya Ndani wa Msumbiji, Amade Miquidade amesema Mei 13, 2020 vikosi vya usalama vya Msumbiji vilifanikiwa kulizingira kundi la wapiganaji 42 wa mgambo waasi wenye ushirika na magaidi; na kuwaua wote.

Ameongeza kuwa Alhamis hii askari wa jeshi la nchi hiyo pia walifanikiwa kuwauwa wapiganaji wengine 8, katika barabara inayoiunganisha miji ya Chinda na Mbau.

Mashambulizi hayo yamepelekea siku za hivi karibuni vikosi vya usalama nchini humo kuwaua wanamgambo takribani 50, katika jimbo la kaskazini la nchi hiyo la Cabo Delgado.

Jimbo hilo linatajwa mara kwa mara kugubikwa na vurugu. Tangu mwaka 2017 majengo ya serikali yamekuwa yakishambuliwa na makundi ya wanamgambo ambayo yanahisiwa kuwa na muungano na kundi la Dola la Kiislamu (ISIS).

Tangu alipoanza Muhula wa Pili, Rais Filipe Nyusi amekuwa akilalamika kutumia fedha nyingi katika kukabiliana na makundi ya wapiganaji.

Corona Uganda: visa 21 vyaongezeka, wote madereva

Mahakama ya Rufani yawaachia huru waliofungwa miaka 20 kwa ujangili

Corona Uganda: Visa 21 vyaongezeka, wote madereva
Mahakama ya Rufani yawaachia huru waliofungwa miaka 20 kwa ujangili