Mtu mmoja nchini Nigeria aliyekuwa amekamatwa kwa kumuita mbwa wake jina la rais Muhamadu Buhari ameachiliwa huru bila ya kushtakiwa mara baada ya kugundulika kuwa hana hatia.
Joe Fortemose Chinakwe alitoa utetezi wake kuwa hakuwa na lengo la kumkashifu rais Buhari alipomwita mbwa wake jina la rais huyo.
”Nilimuita mbwa wangu jina la rais kwa sababu yeye ni shujaa wangu.Nilianza kumpenda Buhari wakati alipokuwa mwanajeshi hadi leo ambapo amekuwa rais.baada ya kuona maamuzi anayochukua dhidi ya ufisadi unaodidimiza uchumi wa taifa hili ,niliamua kulibadilisha jina la mbwa wangu nikamuita Buhari.Sikujua kwamba nilikuwa nafanya makosa kwa kumpenda Buhari”