Jeshi la Polisi, linamshikilia mtuhumiwa wa mauaji ya watu saba aliyejulikaan kwa jina la Peter Morisi (33), katika kijiji cha Kiganza wilaya na Mkoani wa Kigoma.

Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi nchini, Liberatus Sabas imesema Jeshi limejiridhisha kuwa Peter ndiye aliyehusika na mauaji yaliyotokea usiku wa kuamkia Julai 3, 2022 ambapo chanzo chake kinadaiwa ni wivu wa mapenzi.

”Huyu tumejiridhisha bila ya shaka kuwa yeye ndiye aliyehusika na mauaji yale bila ya shaka lakini vielelezo ambavyo amevitumia katika kutekeleza mauji yale navyo vimepatikana sababu ya mauaji haya ni wivu wa kimapenzi,” amesema Sabas.

Aidha, amebainisha kuwa, “Mtuhumiwa huyu alikuwa anamtuhumu marehemu January Mussa (35) amabye pia naye ni mhanga kwenye mauaji hayo kwamab alikuwa anatembea na mke wake na kwasababu hizi zilimpelekea kuingaia hasira na kutekeleza mauaji haya.”

Sabas amesema, taratibu za kipelelezi zinakamilishwa na muda si mrefu mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani kukabiliana na tuhuma za mauaji zinazomkabili.

Waziri Mkuu 'akalia kuti kavu' mawaziri wake wajiuzulu
Mfaume Mfaume: Nilifanya mzoezi kwa miezi mitatu