Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, amefanya ziara katika Mgodi wa Dhahabu wa Shanta uliopo Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida kwa lengo la kukagua usimikaji wa mifumo ya Usalama na Afya katika hatua za awali za maandalizi ya uchimbaji madini katika mgodi huo.

Waziri amesema ni muhimu kwa sehemu mbalimbali za kazi zinazoanzishwa hapa nchini ikiwemo migodi kuwahusisha wataalam wa Usalama na Afya katika hatua za awali za ujenzi wa miundombinu ili waweze kupata ushauri utakaowawezesha kujenga miundombinu salama na isiyo kinyume na sheria.

“Kwetu sisi na wenzangu wa OSHA tutakachojitahidi ni kuendelea kuwapa elimu ya kutosha kuhusu masuala ya usalama na afya mahali pa kazi ili mbobee kwenye eneo hilo kusudi muondoshe migogoro katika eneo lenu la kazi na ndio maana ninaomba muwaruhusu hapa wawe na tawi la wafanyakazi, Lakini tutawasadia pia kukagua na kuangalia mifumo yenu ya usalama na afya kama itaweza kulinda afya za wafanyakazi hususan pale mtakapoanza rasmi uzalishaji,” Amesema Waziri Muhagama.

Akiwasilisha taarifa yake kuhusu hali ya usalama na afya katika mgodi huo mbele ya Waziri, Mkurugenzi wa Usalama wa OSHA, Mhandisi Ngata amesema kampuni hiyo imekuwa ikijitahidi kutekeleza matakwa yote ya Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi kama ambavyo wamekuwa wakielekezwa na wataalam kutoka OSHA.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Kanda ya Kati inayojumuisha mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na Kigoma, Venance Buliga, amesema wamekuwa wakishirikiana ipasavyo na uongozi wa mgodi huo katika hatua mbalimbali za ujenzi wa miundombinu ya uchimbaji madini katika mgodi huo

KMC FC yatepeta ugenini
Dkt. Ndumbaro atoa maagizo kwa watumishi wa Umma