Serikali ya nchi ya Nigeria, inapambana na mafuriko mabaya zaidi kuwahi kutokea katika muongo mmoja baada ya mvua kubwa kunyesha katika eneo hilo, ambapo inaarifiwa takriban watu 20 walikufa ndani ya wiki hii na zaidi ya watu 300 walifariki katika matukio ya mafuriko hadi sasa tangu kuanza kwa mwaka huu 2022.

Mafuriko hayo, yameathiri watu nusu milioni katika majimbo 27, mamia ya watu wakijeruhiwa na takriban zaidi ya watu 100,000 wamelazimika kuyahama makazi yao, huku Shirika la kudhibiti majanga likionya juu ya madhara makubwa katika wiki zijazo kwani mabwawa mawili yameanza kufurika.

Nigeria, ndio nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika ikiwa na zaidi ya watu milioni 206, na inaarifiwa kuwa maji yaliyotokana na mafuriko yameharibu maelfu ya hekta za mashamba, hali inayozidisha hofu ya kukosekana kwa chakula baada ya mimea kusombwa na maji katika eneo lote la kaskazini, ambalo linazalisha sehemu kubwa ya chakula cha nchi hiyo.

Hata hivyo, hali hiyo imetajwa kuzua wasiwasi kwamba inaweza kuathiri zaidi vifaa ambavyo tayari vimetatizwa na vita katika maeneo ya kaskazini magharibi na kati na Shirika la Huduma za Kihaidrolojia la Nigeria linatabiri mafuriko zaidi mwaka wa 2022 kuliko mwaka jana kutokana na uwepo wa mvua nyingi.

Mil 17 wafa kwa magonjwa yasiyoambukizwa
Ruto ataka sentensi mpya mapambano Uviko-19