George Owino Yasin, mgombea kiti cha MCA huko Siaya ambaye alitoweka kwa zaidi ya wiki moja amepatikana katika kaunti ya Kwale akiwa amefumbwa macho na amefungwa kwa kamba kaunti ya Kwale.

Kulingana na ripoti ya polisi ambayo iliyowasilishwa kupitia OB 11/11/05/2022, Rama Janji, chifu wa eneo la Mangawani alipata habari kuhusu mwanasiasa huyo kupitia kwa mmoja wa wanakijiji wake.

Alifahamishwa kuwa kulikuwa na mtu ambaye alikuwa amefumbwa macho na kufungwa kwa kamba ndani ya kichaka katika kijiji cha Mauya.

Wakati maafisa wa polisi wakiongozwa na Stapol Kubo walikimbilia eneo la tukio, ilibainika kuwa mtu aliyezibwa macho alikuwa George Odiwuor Owino.

Yasin alitekwa nyara mnamo Jumatano, Mei 4, na watu wasiojulikana viungani mwa mji wa Ugunja ambao walimlazimisha kuingia ndani ya gari aina ya prado na kuelekea Busia mjini.

“Wamekuwa wakimpeleka maeneo tofauti baada ya kumfumbia macho. Alisema kuwa watekaji nyara hao walidai kuwa wametumwa na mpinzani wake ambaye hawakumtaja,” taarifa hiyo ilisema.

Ripoti hiyo iliongeza kuwa wakati wa kisa hicho, Yasin alipoteza mkoba wake mweusi uliokuwa na KSh 400,000, simu mbili za rununu za Realmi zenye thamani ya KSh 18,000 na Itel Batton yenye thamani ya KSh 2,000 Aidha Yasin pia alipokonywa bidhaa zake zingine ikiwemo kitambulisho cha kitaifa.

Wengine Simba SC kufuata nyayo za Bernard Morrison
Sheikh Mohamud arudia Urais Somalia