Serikali imeshauriwa kuunda tume ya kuchunguza tabia ya baadhi ya Polisi kukwepa gharama za kusafirisha mahabusu kutokana na hali hiyo kuendelea kuwaegemea watu wasiohusika.

Ombi hilo limetolewa na Mbunge wa Muleba Kaskazini (CCM), Charles Mwijage Bungeni hii leo Novemba 9, 2022 wakati alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Amesema, majibu ya Serikali kuwa gharama hizo zinabebwa na watu wa Magereza na Mahakama hazina uhalisia na hali ilivyo kwenye maeneo mengi nchini kutokana na jinsi ambavyo wafungwa wanasafirishwa.

Mbunge wa Muleba Kaskazini (CCM), Charles Mwijage.

Mwijage amefafanua kuwa, “Mwaka jana bibi yangu Juliana Gaesha alikamatwa na kupelekwa Kamachumu lakini ambapo alihukumiwa kifungo lakini Wakati anatoka mshtaki wake alitakiwa kulipia gharama na walibebwa mishikaki.”

Katika swali la msingi mbunge huyo aliuliza juu ya nani anatakiwa kuwagharamia watuhumiwa wa uhalifu wanapokuwa chini ya Polisi hasa wanapotakiwa kwenda mahakamani ambapo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini alijuibu kuwa, jukumu la kugharamia watu hao ni la vyombo husika ikiwemo Polisi na Magereza.

Dkt. Gwajima ataka kasi utekelezaji maendeleo ya jamii
TEF yapendekeza Wavuvi kuandaliwa Jeshi la akiba Uokozi