Nana Akufo-Addo ameapishwa kuwa rais Ghana kufuatia kuibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita, huku akimbwaga aliyekuwa rais wa nchi hiyo John Mahama.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 72, ambaye ni wakili wa zamani wa kutetea haki za binadamu, ameapishwa katika hafla iliyoandaliwa leo kwenye uwanja wa uhuru jijini Accra na kuhudhuriwa na wageni 6,000 na umati mkubwa.

Aidha, Rais huyo mpya amesema kuwa ni lazima kurejesha uadilifu serikalini, na kutahadhalisha kuwa fedha za umma hazipaswi kutumika visivyo na chama kinachoshinda uchaguzi bali kukuza rasirimali za nchi na maendeleo kiuchumi.

Wakuu wa nchi 11 walihudhuria sherehe hiyo akiwemo rais anayeondoka madarakani John Dramani Mahama. Nana Akufo-Addo alimshinda John Mahama katika uchaguzi wa rais mwezi uliopita,

Aidha, kukubali kushindwa kwa Mahama,kumeifanya Ghana kutajwa kama mhimili imara wa demokrasia katika eneo hilo.

Wakenya wamchezesha Nyota Ndogo Muziki wa Darassa, wamuitia pesa
Maafisa uvuvi wazembe kukiona cha moto