Wimbo wa Darassa ‘Muziki’ ambao umekuwa wimbo mkubwa zaidi wa hip-hop kutikiza Tanzania tangu mwaka jana, umeitikisa Kenya na kuwafanya mashabiki kushindwa kuzuia kiu yao katika tamasha la ‘Nyota Ndogo’.

Kwa mujibu wa Nyota Ndogo, mashabiki wake wa Malindi walilipuka kwa shangwe baada ya kumaliza kufanya nyimbo kadhaa wakimtaka ‘DJ’ kuwapigia ‘Muziki’ ya mkali huyo aliyeanza kutikisa nyaya za Mainstream na wimbo wa ‘Sikati Tamaa’.

Mashabiki hao hawakuishia hapo, walimtaka Nyota Ndogo kuonesha mbwembwe za kuucheza Muziki wa Darassa, hali iliyomfanya msanii huyo wa kike kumshtua rapa huyo kuzifuata pesa zake Kenya mapema.

“@darassacmg plz kuna pesa zako kenya zinakungoja.this was my show in malindi.nimemaliza kupiga show mashabiki wanamuomba dj acheze nyimbo yako na mimi ni dance.nipo na video yani mimi ni dance.kimbia huku mara moja kabla nyimbo haijaisha ufanye tour ongea na @gatesmgenge nimzuri wakupiga debe.unamashabiki sio tz pekeake.do it now,” Nyota Ndogo ameandika Instagram na kupost picha ya umati.

kenya-mashabiki

Ilichukua dakika chache kwa jamaa anayetajwa kuwa mzuri wa kupiga debe Kenya anayetumia jina la Gatesmgenge, kuifanyia kazi fursa hiyo ili wagawane pesa na Darassa.

“@nyota_ndogo tayari mpangilio wafanywa tayari tushazungumza na @hanscana_ karibuni watu wangu wa #Malindi” aliandika Gatesmgenge.

Ni kama imethibitishwa Darassa anaenda kuzifuata pesa zake Kenya wakati Afrika ikimsubiri pia kumlipa pesa zake kwa kazi nzuri aliyoifanya.

Lakini sio mashabiki wa kawaida tu waliodata na ‘Muziki’, hata watu maarufu kama Huddah Monroe waliufungua mwaka 2017 kwa kuuonesha ulimwengu kuwa kati ya nyimbo zote duniani ‘Muziki’ ndio wanaotaka kufungua nao mwaka.

+254 Happy new year big shout out to my ambassador @huddahthebosschick unawakilisha vyema ?? #muziki #CMG

A video posted by MagicMusicBoy #CMG (@darassacmg) on


Kubaliana na hoja hii, ‘Darassa hana bahati, ana baraka’.

Diamond kufunika ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2017’
Nana Akufo- Addo aapishwa kuwa rais mpya wa Ghana