Hutuba ya kwanza ya Rais mteule wa Burundi, Evariste Ndayishimiye amesema ushindi wake ni wa raia wote waliomchagua na ambao hawakumchagua.

Akihutubia baada ya kutangazwa mshindi, Ndayishimiye  amemshukuru mtangulizi wake Rais Pierre Nkurunziza kwa hatua yake ya kuridhia kuanzisha mchakato wa uchaguzi.

Kiongozi huyo wa chama cha CNDD-FDD aliyeibuka mshindi uchaguzi wa Mei 20 ameongeza kuwa uchaguzi huu umedhihirisha kukuwa kwa umahiri wa kisiasa wa Burundi ambapo ameahidi kuwasikiliza raia wote Burundi bila ubaguzi.

“Tumejipa hadhi mbele ya Warundi na dunia, kwa kuionesha kuwa tulipofikia hatufundishwi tena demokrasia bali tunaweza kuwafundisha wengine hivyo ninaahidi kuwa nitawasikiliza wananchi wote bila ubaguzi, hivyo naitaka jumuia ya kimataifa kuiunga mkono hatua hii ya kupendeza tuliyoifikia”. amesema Rais Ndayishimiye

Ndayishimiye anayefahamika kwa jina la utani kama ”Neva” alihudumu katika jeshi kwa muda mrefu kabla ya kujiunga katika siasa, alikuwa mwanafunzi mdogo katika chuo kikuu cha Burundi mwanzoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo mwaka 1993.

Watanzania 16 wakutwa na Corona Uganda
RC Chalamila akagua maendeleo ya utalii fukwe za Ziwa Nyasa

Comments

comments