Tume ya Uchaguzi (NEC), imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Muhambwe (CCM), Dkt. Florence George Samizi, dhidi ya Mgombea wa ACT-Wazalendo, Masabo Julius Joseph, ikisema anaweza kuendelea kuwepo katika Uchaguzi

Katika pingamizi la kutoambatanisha picha zenye mwonekano wa rangi nyeupe kwa nyuma, NEC imesema haikuwa sababu ya pingamizi kwa mujibu wa Sheria.

Aidha, kuhusu hoja kuwa saini za Wadhamini zimeghushiwa, NEC imesema imeshindwa kuthibitisha hilo na hakutaja majina ya Wadhamini anaodai saini zao zimeghushiwa.

Jimbo la Muhambwe linafanya Uchaguzi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Atashasta Nditiye aliyefariki Februari mwaka huu.

Kocha Gomez afichua siri ya mafanikio Simba SC
Rais Samia atoa msimamo kuhusu Corona, "hatuishi kwenye kisiwa"