Hatimae mshambuliaji wa FC Barcelona, Neymar da Silva Santos Júnior, amemaliza kifungo cha kutocheza michezo minne, kilichomuangukiwa wakati wa fainali za mataifa ya kusini mwa Amerika (Copa America) zilizorindika nchini Chile miezi minne iliyopita.

Neymar, alifungiwa na  shirikisho la soka katika ukanda huo, na adhabu hiyo kupewa baraka na FIFA, baada ya kuanzisha ugomzi wakati wa mchezo wa Copa America dhidi ya Colombia ambao walichomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri.

Tayari mshambuliahi huyo mwenye umri wa miaka 23, ameshatajwa kwenye kikosi kitakachocheza, michezo ya kimataifa ya kuwania kufuzu fainali za kombe al dunia za mwaka 2018, dhidi ya Argentina pamoja na Peru itakayochezwa mwezi ujao.

Kikosi cha Brazil, tayari kimeshapoteza michezo miwiwli ya ufunguzi katika kampeni za kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia, baada ya kukubali kufungwa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Chile na kisha kupoteza mbele ya Venezuela, kwa kufungwa mabao matatu kwa moja, mwezi huu.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil, Carlos Dunga anaamini kurejea kwa mshambuliaji huyo ambaye pia ni nahodha wa kikosi chake, huenda kukaleta chachu na kuanza kupata ushindi kwenye michezo ya mwezi ujao.

Hata hivyo Dunga ambaye aliwakua sehemu ya wachezaji waliokau wanaunda kikosi cha Brazil kilichotwaa ubingwa wa dunia mwaka 1994 kule nchini Marekani, amekiri bado kuna upinzani mkali katika michezo hiyo miwiwli, hivyo hana budi kujipanga vyema.

Wengine walioongezwa kwenye kikosi cha Brazil, tayari kwa michezo dhidi ya Argentina na Peru, ni mlinda mlango, Cássio Roberto Ramos  sambamba na beki Carlos Gilberto  pamoja na viungo Elias Mendes na Renato Augusto ambao wote wanatokea kwenye klabu ya Corinthians.

Wengine ni Lucas wa Paris St. Germain, pamoja na Philippe Coutinho wa Liverpool.

Kesi Ya Mita 200: Swali La Jaji Kwa Wakili Kibatala Lamgusa Mbowe
Dynamo Kiev Kusimamishwa Mahakama Ya UEFA