Mwanamuziki maarufu wa Hip Hop hapa nchi Nikki Mbishi, amempongeza msanii wa bongo fleva Rajabu Abdul maarufu kama Harmonize, kwa kuamua kutafuta maisha ya kujisimamia mwenyewe katika tasnia ya muziki.

Akizungumzia hilo kupitia ukurasa wake wa instagram Nikki alisema kuwa Harmonize ni miongoni  mwa wasanii  waliopiga hatua  kutoka WCB , lakini ameamua kutoka kwenye lebo hiyo baada ya  kujiona mwenyewe anaweza.

”kiukweli nampongeza sana  Harmonize kwa hatua aliyofikia kwani wapo wanamuziki wengi wanapokuwa kwenye lebo yoyote wanashindwa kujiamini ili kutafuta maisha yao binfsi ” aliandika Nikki

Hata hivyo msanii huyo aliwalaumu wakongwe wa muziki ambao kwa sasa ni wabunge katika baadhi ya mikoa hapa Tanzania Joseph Mbilinyi, maarufu kama ‘Sugu’ na mbunge wa Mikumi Professor Jay, wangekuwa  ma wakurugenzi wa kampuni kubwa za muziki hapa nchi lakini hawajaweza kufanya hivyo.

Walioua kwa mil. 1, wahukumiwa kunyongwa hadi kufa
Mashabiki Arsenal wamtaka Unai Emery ajiuzulu