Claudio Bravo sasa anatarajiwa kujiunga na Manchester city na kuchukua nafasi ya Joe Hart ambaye anaonekana kutokuwa na nafasi tena chini ya kocha Pep Guardiola.
Tangu alipotua klabuni hapio, Guardiola alionekana kuhitaji kumsajili kipa huyo, ambaye aina ya uchezaji wake unafanana na mlinda lango wa Bayern Munich Manuel Neuer.
Bosi huyo wa zamani wa Barcelona ameonekana kumpata mtu sahihi kutokana na mahitaji yake, na takwimu za kipa huyo zinamfanya Joe Hart kutokuwa na nafasi tena mbele ya Guardiola. Bravo ana uwezo mkubwa wa kuchezea mpira kuliko Hart.
Ndani ya miaka mitatu, mchezaji huyo wa zamani wa Real Sociedad amecheza pasi fupi 1,310 ambazo kwa mujibu wa mtandao wa Opta hazizidi umbali wa hatua 25.
Tofauti na Joe Hart ambaye amecheza pasi 562. Hart amecheza mipira mirefu 1,674 tofauti na Bravo ambaye amecheza 1,363.
Kwa maana hiyo, robo tatu ya pasi za Hart ni ndefu ukilinganisha na Bravo ambaye ni asilimia 51 tu ya pasi zake ndio ndefu
Bila shaka kwa takwimu hizo, Bravo anaonekana kuwa mtu sahihi kwa aina ya mfumo wa Guardiola kuliko Joe Hart, na je, vipi kuhusu utimamu wa pasi hizo (passing accuracy)?
Wastani wa pasi fupi za Bravo zilizofanikiwa kufika sehemu husika ni asilimia 99 huku Hart akipata asilimia 97.
Kwa upande wa pasi ndefu, Bravo anapata asilimia 49, wakati Hart anapata asilimia 33.

Mr Blue amfananisha Baraka Da Prince na Bajaji, “hawezi kugongana na Meli”
Coastal Union Kuzibana Simba, Yanga, Kagera Sugar Na Mbeya City