Mkuu wa Wilaya Geita, Herman Kapufi amepiga marufuku mikesha ya dini na upigaji muziki usiku wa manane kutokana na mauaji ya walinzi yanaoendelea kutokea wilayani humo.

Wilaya hiyo imekuwa na matukio ya mauaji ya walinzi mfululizo huku mwaka mmoja, walinzi 18 kutoka kampuni binafsi wameuawa.

Alisema hakuna baa, nyumba ya starehe au nyumba za ibada zitakazoruhusiwa kuendelea na shughuli yeyote baada ya saa tano na watakaokuwa na uhitaji itawaradhimu kuomba kibali maalumu kwa siku husika.

”Haya mauaji yanatisha kwani wanaoua hawachukui chochote jambo lililowasababisha wananchi wahusishe mauaji haya na imani za kishirikina” Alisema Herman Kapufi.

Mwenyekiti wa kampuni za ulinzi wilayani hapo Ayoub Mwita , alisema kitendo cha jeshi la polisi kuzuia walinzi binafsi kutumia silaha za moto ni moja ya sababu zinanzochangia mauaji kutokea kwa kuwa wanashindwa kupambana na wavamizi.

Alisema sababu myingine ni makampuni kuajili vijana wasio na mbinu  za kujilinda kwa sabau hawajapitia mafunzo ya mgambo hivo ni vyema serikali ikaweka mkazo katika suala la kuajiri watu wenye uzoefu.

 

Angelina Jolie amtoa chozi Brad Pitt, ampa adhabu nyingine nzito baada ya kumtosa
Video: Mechi Wabunge Simba, Yanga yachangia sh. Mil. 187 waathirika tetemeko la Kagera