Bodi ya Rufaa za Kodi (Trab) inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu kesi ya Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka anayepinga tozo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya shilingi milioni 586 kutokana na mgawo wa shilingi bilioni 1.62 alizopokea kutoka kwenye akauti ya Tegeta Escrow.

Trab, imepanga kutoa hukumu ya keshi hiyo Machi 29 mwaka huu ambapo Profesa Tibaijuka ambaye alikuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika serikali ya awamu ya nne kabla hajaondolewa kutokana na sakata la fedha hizo, atajua hatima yake kuhusu malipo anayodaiwa na Mamlaka hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa Trab, Hakimu Agusta Mmbanddo ameipanga tarehe hiyo ya kutoa maamuzi baada ya kumalizika kwa hatua ya kusikiliza pande zote mbili zilizokuwa zikivutana katika kesi hiyo.

Rufaa hiyo ilisikilizwa na Hakimu Mmbando Februari 17, 19 na 22 wakati Profesa Tibaijuka alipokuwa akitoa ushahidi.

Profesa Tibaijuka, alidaiwa kupokea kiasi cha shilingi bilioni 1.62 kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, ambayo iliundwa kusubiri utatuzi wa mgogoro wa malipo ya ununuzi wa umeme kati ya Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), na Kampuni ya Kufua Nishati ya Umeme (IPTL).

Profesa Tibaijuka alikiri kupokea fedha hizo huku akieleza kuwa alipewa kwa ajili ya matumizi ya shule, ingawa kumbukumbu za kibenki zilionesha kuwa fedha hizo ziliwekwa kwenye akaunti ya shule na kuondolewa muda mfupi baadae.

 

 

Maalim Seif arejea kutoka India, arusha jiwe la kwanza kwa Polisi
Wamiliki wa Jamii Forum watinga mahakamani