Hatimaye Rais wa Marekani, Barack Obama amekutana na Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte na kufanya nae mazungumzo mafupi, ikiwa ni siku chache tangu aahirishe mkutano wao huo.

Awali, Rais Obama alipanga kukutana na Rais huyo wa Ufilipino lakini aliahirisha baada ya kiongozi huyo kumuita ‘mtoto wa kahaba’.

Taarifa zimeeleza  kuwa wawili hao walifanya mkutano huo mfupi jana walipokutana katikma mji mkuu wa Vientiane nchini Laos, kabla ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa eneo la Kusini Mashariki mwa bara la Asia.

Hata hivyo, wawili  haikufahamika mara moja walichozungumza viongozi hao.

Sintofahamu kati ya viongozi hao iliibuka baada ya Obama kueleza kuwa atakapokutana na rais huyo wa Ufilipino kuhusu mauji ya kihlolea ya watuhumiwa wa biashara ya madawa ya kulevya. Kiongozi huyo wa Ufilipino alijibu kuwa endapo atamuuliza swali hilo atamtukana huku akimuita ‘mtoto wa kahaba’.

Rais huyo wa Ufilipino ambaye mara kadhaa matamshi yake yamezua utata alidai kuwa nchi hiyo ni huru na haitawaliwi na Taifa lolote duniani. Alirejea hayo kwakuwa Ufilipino iliwahi kuwa koloni la Marekani.

Video: Serikali kuboresha nyumba za kurekebishia tabia watoto
Mahakimu 11 watumbuliwa, 34 wawekwa kiporo