Seneta wa Ufilipino na bingwa wa zamani wa ndondi, Manny Pacquiao anatarajia kupanda ulingoni saa chache zijazo na bondia machachari mwenye asili ya Mexico, Jessie Vargas.

Pacquiao ambaye anapanda ulingoni kwa mara ya kwanza tangu awe Seneta wa ‘Baraza la Mawaziri’  la nchi yake, ataweka rekodi mpya kwenye historia ya mchezo huo kwa kuwa Seneta wa kwanza kuzichapa ulingoni.

Vargas ambaye ni kijana mdogo wa miaka 27 anaezidiwa miaka kumi na Pacquiao, atautetea mkanda wa ubingwa wa dunia wa WBO wa uzito wa Welterweight akiahidi kuweka historia ya kumpiga nguli huyo kwa namna ya kushangaza.

Pambano hilo litafanyika katika ukumbi wa Thomas & Mack Center, Las Vegas, Navada nchini Marekani, ambapo kwa saa za Afrika Mashariki itakuwa Jumapili Alfajiri.

“Nina uhakika nitashinda kwa sababu nimejiandaa vizuri. Nina kila sababu ya kushinda kwa sababu nataka kuwa Bondia mkali Zaidi. Najua kuwa mkali Zaidi lazima umpige mkali zaidi. Pacquiao alikuwa ndiye mkali zaidi,” alisema Vargas.

Naye Pacquiao ambaye alikuwa ametangaza kustaafu masumbwi na kurejea tena, alisema “nimerejea ulingoni na nina kila kitu cha kuthibitisha. Nataka kuweka historia ya kuwa Seneta wa kwanza kuwa Bingwa wa dunia wa masumbwi.”

 

Bunge lapitisha Muswada wa sheria ya huduma za habari
Wasomi wachambua msimamo wa Magufuli kuhusu katiba mpya