Hatimaye Bunge la Austria limefanikiwa kupitisha sheria itakayoiwezesha Serikali ya nchi hiyo kulimiliki jumba la kihistoria alilozaliwa kiongozi wa zamani wa Ujerumani, Adolf Hitler aliyeongoza vita ya pili ya dunia (WWII) dhidi ya Uingereza na marafiki zake.

jumba-la-hitler

Hitler alizaliwa katika jumba hilo Aprili 20 mwaka 1889, katika chumba cha ghorofa ya juu kilichopangishwa na wazazi wake. Wakati wa utawala wake, sehemu ya jumba hilo alipozaliwa lilibadilishwa kuwa madhabahu yaliyovutia watu wengi.

Serikali imekuwa ikitafuta njia ya kuweza kulimiliki jumba hilo kutokana na mmiliki wake, Bi. Gerlinde Pommer kukataa kuiuzia Serikali na hata kulikarabati.

Serikali ya Austria imekuwa ikihofia kuwa jumba hilo linatumika kama kumbukumbu ya kuwatia moyo wafuasi wa kiongozi huyo wa chama cha Ki-Nazi aliyeiongoza Ujerumani tangu mwaka 1934 hadi 1945.

Bi. Pommer sasa atalipwa fidia na kuliachia jumba hilo mikononi mwa Serikali ambayo hata hivyo haijaweka wazi italifanyia nini.

Mnyama Afunga Safari, Awafuata Ndanda FC
Kinnah Phiri Kukamilisha Usajili Usiku, Ngassa Mambo Safi