Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga jana liliuthibiti msafara wa viongozi wa Chadema uliokuwa ukiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe usifanye shughuli zozote za kisiasa mkoani humo ulipokuwa ukitoka Shinyanga kuelekea jijini Mwanza.

Magari manne ya Jeshi hilo yakiwa na askari yaliusindikiza msafara huo hadi nje ya mkoa na kuwazuia viongozi hao kuingia katika ofisi za chama hicho kusaini kitabu cha wageni.

Viongozi waliokuwa katika msafara huo pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho, ni Katibu wake, Dk. Vicent Mashinji na wabunge Godbless Lema, Ester Bulaya, John Heche, Halima Mdee na wengine.

Jumatatu, Jeshi la Polisi nchini lilipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa pamoja na maandamamo nchini kwa sababu za kiusalama hadi pale litakapotoa taarifa vinginevyo.

Chadema na ACT-Wazalendo kwa nyakati tofauti wamepinga hatua hiyo ya Serikali na kuazimia kudai haki ya kufanya mikutano hiyo kwa nguvu zote ikiwa ni pamoja na kwenda Mahakamani kuomba tafrisi ya sheria.

Southampton Wamgeukia Frank De Boer
Huenda Kikosi Hiki Ndicho Bora Kwa Msimu Wa 2015-16