Waziri wa Maji na Umwagiliaji Tanzania, Prof. Makame Mbarawa amewasili Ofisi Kuu za CCM kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais na alikuwa Mgombea wa 10 kuchukua fomu visiwani Zanzibar.

Katika hatua nyingine, mama Mwantum Mussa Sultan anakuwa Mwanamke wa kwanza kuchukua fomu ya Urais kwa tiketi ya CCM na ni Mwanachama wa 11 kujitokeza kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais Zanzibar

Wengine waliochukua fomu ni Mbwana Bakari Juma, Ali Abeid Karume, Mbwana Yahya Mwinyi, Dkt. Hussein Mwinyi, Omar Sheha Mussa, Shamsi Vuai Nahodha, Mohamed Hija Mohammed, Mohammed Jaffar Jumanne na Balozi Meja Jenerali Mstaafu Issa Suleimani Nassor.

Zoezi la utoaji fomu linaendelea katika Ofisi Kuu za CCM zilizopo Kisiwandui na linatarajiwa kukamilika Juni 30,2020.

Wagonjwa mikoani kutibiwa MOI kwa mtandao
DC aagiza Baba aliyewabaka watoto wake watatu kukamatwa