Wakati vita kati ya Ukraine na Urusi ikiwa bado inaendelea, nchi hiyo imesalia bila umeme baada ya Vikosi vya Urusi kushambulia kwa makombora gridi ya taifa.

Wakazi wa Kyiv, wametahadharishwa kujiandaa kwa mashambulizi zaidi na wajihami kwa maji, chakula na nguo nzito.

Raia nchini Ukraine. Picha ya CNBC.

Hata hivyo, Urusi imekiri kwamba imeishambulia miundo mbinu ya kimsingi ya Ukraine kupunguza uwezo wa Ukraine kupambana na kuisukuma katika meza ya majadiliano.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky pia ameituhumu Urusi kufanya msururu wa mashambulizi katika eneo la Kherson, mji ulio kusini mwa nchi hiyo ambao ulikombolewa mwezi huu (Novemba, 2022).

Tunajenga Chuo cha Mafuta, Gesi na Umeme: Makamba
Wenye nyumba, wapangaji kulipwa fidia Jangwani