Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila leo amewasili nchini kwaajili ya ziara ya kiserikali  ya siku tatu na kupokelewa na mwenyeji wake rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli   uwanja wa ndege wa mwalimu Julius kambarage nyerere jijini Dar es salaam.

Rais kabila mara baada ya kuwasili amepata heshima ya kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwaajili yake na baadaye kushuhudia burudani ya vikundi vya ngoma,

Aidha rais kabila anatarajia kufanya mazungumzo na mwenyeji wake rais Magufuli hapo kesho na baadaye kuzindua rasmi jiwe la msingi la jengo la mamlaka ya bandari tanzania (TPA) na baadaye kushiriki dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na mwenyeji wake rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dkt.John Magufuli

Video: Taarifa ya Kamanda Sirro kuhusu kukamatwa kwa Jambazi sugu Dar
Video: Polisi Dar kuwakamata waliofanya vurugu mechi ya Simba na Yanga