Rais John Magufuli ambaye ametajwa kuwania tuzo ya mtu mashuhuri barani Afrika kwa mwaka 2016 (Forbes Africa Person of the Year) inayotolewa na jarida la ‘Forbes Africa’, ameonesha dalili za ushindi mapema akiongoza kwa kishindo kwa idadi ya kura zilizopigwa.

Hadi leo mchana, Rais Magufuli alikuwa akiongoza kwa asilimia 84 dhidi ya washiriki wenzake ambao ni watu mashuhuri Afrika pamoja na watu wa Rwanda (Taifa la Rwanda).

Wakieleza sababu za kumjumuisha Rais Magufuli kwenye orodha ya wanaowania tuzo hiyo mwaka huu, Forbes wamesema, “Rais huyu wa Tanzania amefanya kazi kubwa ya kuinua uchumi wa nchi.”

Wengine wanaowania tuzo hiyo ni Rais wa Mauritius, mwana mama shupavu Ameenah Gurib ambaye ametajwa kuingia kwenye orodha hiyo kutokana na jitihada zake za kulinda mazingira. Aliwahi kutajwa na Forbes kuwa kati mwanamke mwenye nguvu zaidi (ushawishi) duniani akishika nafasi ya 96 kwa mwaka huu.

Afrika Kusini wana washiriki wawili ambao ni Mwendesha Mashtaka maarufu, Thuli Madonsela ambaye jitihada zake za kupambana na rushwa zimetambulika, pamoja na mwanzilishi wa Benki ya Capitec, Michiel le Roux.

Mwaka jana, Mfanyabiashara mtanzania Mohammed Dewji ndiye aliyeshinda tuzo hiyo akipokea kijiti cha bilionea wa Nigeria, Aiko Dangote aliyeshinda tuzo hiyo mwaka 2014.

mo-dewji

Mohammed Dewji baada ya kupokea tuzo ya Forbes mwaka jana

Kumpigia kura Rais Magufuli bofya HAPA

Laurent Blanc Kuchukua Nafasi Ya Frank De Boer?
Lowassa aumulika mwaka mmoja wa Magufuli, 'maisha yamezidi kuwa magumu'