Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Meya Msataafu wa jiji la Dar es salaam, Dk. Didas Masaburi aliyefariki dunia jana  Oktoba 12, 2016 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

Rais ameeleza kupokea taarifa za kifo cha Dk. Masaburi kwa mshtuko na masikitiko makubwa, hivyo anaungana na familia ya maehemu, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha huzuni ya kuondokewa na mpendwa wao.

Magufuli amesema anajua huu ni wakati mgumu kwa familia, hivyo amewahakikishia kuwa pamoja nao kwani yeye pia ameguswa na msiba huo kwa kumpoteza mtu muhimu, msomi mzuri, kiongozi aliyelitumika Taifa kwa moyo wake wote na aliyesimamia kile alichokiamini.

Rais Magufuli pia ametoa pole kwa wapenzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao mwana CCM mwenzao, pamoja na viongozi na watumishi wa jiji la Dar es salaam ambao walifanya nae kazi alipokuwa Meya wa jiji.

“Bwana alitoa na Bwana ametwaa , jina lake lihimidiwe. Amina” amemalizia Rais Magufuli

Wenger Awakataa Wachezaji Vijana, Asema Walimpotezea Muda
DC Mjema Kutatua kero za Wananchi kata za Mvuti na Msongole