Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, amesema Hayati Dkt. John Magufuli alikuwa mstari wa mbele katika kuimarisha maisha ya Watanzania kwa misingi ya Haki na Usawa bila kujali Dini, Kabila, Rangi au Jinsia.

Akizungumza katika tukio la kuaga mwili wa Hayati Dkt John Pombe Magufuli lililofanyika Uwanja Amaan Visiwani Zanzibar, Rais Mwinyi amesema, “Tumempoteza Mwanamapinduzi mahiri wa karne ya sasa. Alikuwa Kiongozi mwenye uwezo na kipaji cha aina yake. Kiongozi kama yeye ni nadra sana kupatikana.”

Katika hotuba yake, amemuelezea Dkt. Magufuli kama Kiongozi aliyejipambanua kwa uzalendo wa kweli, mtetezi wa wanyonge, mwenye kujivunia na kujionea ufahari Utanzania na Uafrika wake

Mwinyi amesema kifo cha Dkt. Magufuli kimeleta simanzi kwa Watanzania na wapenda Maendeleo katika bara la Afrika.

Al Merrikh yamvutia kasi Aishi Manula
Kocha Gomes awahusia wachezaji Simba SC