Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara amemsamehe mtangulizi wake, Laurent Gbagbo ambaye alikuwa anakabiliwa na kifungo cha miaka 20 jela kwa machafuko ya kisiasa.

Katika taarifa yake ya Agosti 6, 2022 ya kuadhimisha miaka 62 ya uhuru wa nchi hiyo, Ouattara alisema hatua hiyo ni kwa ajili ya kuimarisha mshikamano wa kijamii unaolenga amani ya Taifa hilo.

Ouattara, pia aliomba akaunti za benki za Gbagbo zilizokuwa zimefungwa zifunguliwe na malipo yake ya kiinua mgongo yaanze kulipwa kulipwa.

Rais wa Ivory Coast, Alassane Outarra (picha na tovuti ya Wizara ya Maji na Misitu, Ofisi ya Waziri Plateau РIvory Coast/ photo et des Eaux et For̻ts Cabinet du Ministre Plateau).

Gbagbo, alikua rais wa Ivory Coast mwaka 2000, lakini alikamatwa mwaka 2011 baada ya kukataa kukubali kushindwa katika uchaguzi huo.

Mzozo wa wenyewe kwa wenyewe kati ya vikosi vya Gbagbo na wafuasi wa Ouattara, ulisababisha vifo vya karibu watu 3,000.

Gbagbo, aliachiliwa huru na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), kwa tuhuma za uhalifu wa kivita aliotenda wakati wa mzozo huo.

Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara (kulia), akiwa na mtangulizi wake Laurent Gbagbo (kulia). (picha na Africanews).

Mwaka 2018, alihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela, kwa wizi wa pesa kutoka kwa benki kuu ya Abidjan baada ya uchaguzi, madai ambayo amekuwa akiyakanusha.

Hata hivyo, Rais Ouattara pia alikubali kuwaachilia huru washirika wawili wa karibu wa Gbagbo ambao walipatikana na hatia kwa jukumu lao la kushiriki machafuko baada ya uchaguzi.

Aidha, mwaka wa 2021, baada ya kuachiliwa huru na ICC, Gbagbo alirejea kutoka uhamishoni Ivory Coast na amekuwa mkimya tangu wakati huo.

Mstaafu wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo (picha na Flatmat info/ Patrick N’Guessan).

Katika hatua nyingine, wakosoaji wamemgeukia Ouattara ambaye aligombea muhula wa tatu wa uongozi katika uchaguzi wa 2020, hatua ambayo wanadai ni kinyume na katiba.

Rais Ouattara, hata hivyo amesisitiza kuwa hataachana na siasa hadi hapo Gbagbo na mtangulizi wake Henri Konan Bédié nao wakubali kujitenga na siasa.

Waziri atoa saa 48 RC amkamate Mkurugenzi
Bodaboda kuwasafirisha Wazee, Wagonjwa vituo vya kura