Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuapisha Jenista Mhagama kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam hii leo Aprili 2, 2023.

Uapisho wa Jenista Mhagama unafuati uteuzi uliofanywa na Rais Samia ili kuchukua nafasi ya George Boniface Simbachawene na kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan pia George Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Aprili Mosi, 2023 Rais Samia alifanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kwa kumteua Jenista Mhagama kuwa Waziri wa Wizara hiyo na George Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ambapo kabla ya uteuzi huo Simbachawene alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Kifo mikononi mwa Polisi: IGP apeleka timu Chato
Ubadhirifu ripoti ya CAG: Wahusika kuchukuliwa hatua