Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaSamia Suluhu Hassan ameziagiza taasisi za fedha nchini kujadili, kuja na mapendekezo ya haraka kwa Serikali, ya namna ya kuimarisha uchumi ulioporomoroka kutokana na janga la UVIKO – 19.
 
Ameyasema hayo leo Novemba 25, 2021 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa 20 wa taasisi za fedha nchini, ulioandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
 
Amezitaka taasisi hizo za fedha nchini kujadiliana na kuandaa mikakati  haraka iwezekanavyo, itakayosaidia kupunguza umaskini nchini.
 
Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amezitaka benki za biashara nchini kuongeza ubunifu na kupeleka wizarani mapendekezo ya kisera,  ili wizara hiyo  iweze kuongeza utoaji wa mikopo kwenye sekta binafsi hasa katika  maeneo makubwa kiuchumi.
 
Kauli mbiu ya mkutano huo wa 20 wa taasisi za fedha nchini uliojumuisha  wadau wa masuala ya fedha kutoka ndani na nje ya nchi ni “Ukuaji wa uchumi endelevu wakati na baada ya UVIKO – 19, vipaumbele na sera mbadala”.

Nondo za Mwana Fa, kukwama kwa muziki wa Bongo
Wafugaji kulima malisho