Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ameagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mwanga, Zefrin Lubuva asilipwe mshahara wa Februari hadi atakapojirekebisha.

Agizo hilo limetolewa baada ya mkurugenzi kushindwa kujibu kwanini Halmashauri hiyo imeshindwa kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya Wanawake, Vijana na Walemavu.

“Mkurugenzi wa Mwanga kila wakati umekuwa ukishindwa kujibu maswali vile inavyopaswa, sijajua ni nani anakulipa mshahara, ila mamlaka inayohusika kukulipa isikulipe mshahara wa mwezi huu”.

Ikumbukwe kuwa kila Halmashauri nchini Tanzania hutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya kuwapa mikopo isiyo na riba Vijana, Walemavu na Wanawake.

Muumini mbaroni kwa kuiba sadaka kanisani
Chama cha Madaktari kuteta na Magufuli ukosefu wa ajira

Comments

comments