Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete (CCM),amepongeza jitihada zinzofanywa na wataalamu wa Halmashauri ya Chalinze katika kuboresha mradi wa maji wa Wami kwaajili ya wananchi wa Chalinze.

Ametoa pongezi hizo mara baada ya kutembelea mradi huo, amesema kuwa mradi huo ambao ulianzishwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Rais mstaafu  wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete,umekuwa ni mkombozi wa wakazi wa jimbo hilo.

Aidha amesema kuwa lengo la kufanya ziara hiyo katika eneo la mradi huo ni kuona shughuli zinazofanywa na wataalamu kwaajili ya  kuendelea kuboresha  mradi huo.

“Nimefurahishwa sana na jitihada zinazoendelea kufanywa na wataalamu wa Halmashauri hii kuhakikisha wananchi wanapata maji”amesema Ridhiwani.

Hata hivyo ameongeza kuwa kazi kubwa kwake ni kuendelea kuisimamia Serikali kwa kuwawakilisha wananchi vyema Bungeni  kwa kufikisha kero zinazo wakabili ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi

TRA yatoa somo kwa madalali wa Bima
Magufuli asimulia rozali ya ‘sister’ ilivyompa ushindi wa urais