Klabu ya Everton  italazimika kuvunja mkataba wa meneja kutoka nchini Uholanzi Ronald Koeman na klabu ya Southampton kwa kutoa kiasi cha Pauni milion 5, ili kukamilisha mchakato wa kumuhamishia Goodson Park.

Hatua ya kuvunjwa kwa mkataba wa pande hizo mbili, imefikiwa baada ya uongozi wa klabu ya Southampton kuridhia kumuachia Koeman ambaye tayari alikua ameshagoma kusaini mkataba mpya tangu mwishoni mwa msimu wa 2015-16, ambao ulifikia tamati mwezi uliopita.

Koeman, mwenye umri wa miaka 53, amekuwa chaguzo la kwanza la Everton katika mchakato wa kumsaka mbadala wa aliyekua meneja wa klabu hiyo Roberto Martinez ambaye alifukuzwa juma moja kabla ya msimu uliopita kufikia kikomo.

Sifa kubwa iliyompa nafasi ya Koeman kuwa kinara wa mchakato wa kupewa ajira huko Goodson Park, ni mwenendo mzuri alionao katika klabu ya Southamton ambayo imekua ikifanya vizuri tangu ilipofanikiwa kupanda daraja msimu wa 2012-13.

Koeman, alifikia hatua ya kugoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea na Southampton kwa kutoa sharti la kutaka kuhakikishia mustakabali wa baadhi ya wachezaji waliokua wamesalia kikosini, kwa kuhofia huenda wangekuwa sehemu ya kusajiliwa na klabu nyingine kama ilivyokua kwa baadhi ya walioondoka misimu miwiwli iliyopita.

Wakati wa utawala wa meneja huyo wa kidachi, Southampton ilikubali kuwaachia wachezaji kama Nathaniel Clyne pamoja na Morgan Schneiderlin walioondoka mwanzoni mwa msimu wa 2015-16, Rickie Lambert, Luke, Shaw, Adam Lallana, Dejan Lovren na Calum Chambers waliondoka mwanzoni mwa msimu wa 2014-15.

Picha: Madiwani Kilwa na Ruagwa wapigwa msasa
Zoezi La Usajili Wa Zlatan Ibrahimovic Lasitishwa