Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema Jeshi hilo linawashikilia watu saba kwa tuhuma za mauaji ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Joachimu Mwakyolo.

Kuzaga amesema, tukio hilo lilitokea Januari 20,2023 katika kijiji cha Kibole kata ya Itete Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya, ambapo Mwakyolo na mwenzake ambaye jina lake halijafahamika wanadaiwa kuuawa na wananchi.

Amesema, ”Baada ya kikosi maalumu cha upelelezi kukagua eneo la tukio palikutwa mawe ambayo yalitumika kutenda tukio hilo la mauaji pamoja na pistol aina ya CZP – 07 MEC D005150 ikiwa na magazine mbili ambazo zote zilikuwa hazina risasi.”

Aidha, Kamanda kuzaga amesema uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea na wahusika watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Watanzania hunywa Chai daraja la tano
Brazil, Argentina zakusudia kuwa na sarafu moja