Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Tanzania ipo salama akisema ni kawaida kwa Mwanadamu kukaguliwa kaguliwa na mafua, homa na maradhi mengine.

Samia ameyasema hayo akizungumza na Wananchi akiwa Handeni, Mkoani Tanga, ambapo amesema huu ni wakati muhimu kwa Watanzania kushikamana na kujenga Umoja akisisitiza sio wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje.

Ameongeza, “Watu wote shughulikeni na mambo yenu, jengeni Taifa, tujenge Umoja na Mshikamano wetu ili Tanzania iwe Taifa imara, na ndicho kinachotuchongea, uimara wa Taifa letu unaleta maneno mengi.”

Makamu wa Rais leo ameanza ziara ya siku Sita Mkoani humo ambapo atakagua shughuli za maendeleo na kuzindua miradi mbalimbali.

Wafungwa wapigwa 'stop' kazi binafsi
Museveni akishtumu Chama cha Bobi Wine kuiba kura